Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha kupitia taarifa za mechi za Ligi Kuu imeipiga Alliance Girls faini ya Sh500,000 na kupoteza mchezo dhidi ya Yanga Princess kwa kosa la kufanya udanganyifu wakumchezesha mchezaji raia wa kigeni, Oruko Amutata Noel kwa kutumia jina la Shamsa Julius huku wakifahamu kuwa hakuwa sehemu ya usajili wa timu hiyo
Taarifa iliyotolewa kamati mapema leo, imeongeza kuwa Meneja wa Alliance, Oliva Moshi amefungiwa miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Sh500,000 uamuzi uliotolewa kwa kuzigatia Kanuni ya 47(13) ya Ligi za Wanawake
Aidha kaimu Katibu Mkuu wa Alliance, Suzan Geofrey amefungiwa miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Sh 500,000. Uamuzi uliozingatia Kanuni ya 47(13) ya Ligi za Wanawake
Timu ya Yanga Princess imepewa ushindi wa mabao 3-0 kwa kuzingatia Kanuni ya 42 (11) ya Ligi za Wanawake.
Mchezo huo uliopigwa duru ya kwanza ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana