Arafat asisitiza, HATUCHEZI NG'O

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 May 2025
Arafat asisitiza, HATUCHEZI NG'O

Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji, alizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya CRDB FA Cup uliofanyika Jumapili, May 18 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Ushindi huo umeipeleka Yanga SC katika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya tano mfululizo, jambo linalodhihirisha uimara na uthabiti wa klabu hiyo katika soka la Tanzania.

Akiwa na furaha ya mafanikio hayo, Arafat aliwapongeza wapinzani wao, JKT Tanzania, kwa upinzani waliouonesha, huku pia akigusia hali ya uwanja wa Mkwakwani ambao licha ya kufanyiwa maboresho haukuwa kwenye hali nzuri kutokana na mvua iliyonyesha

"Tulijiandaa vizuri kwa yote. Tunamjua mpinzani na tuliujua uwanja ambao pia umetoka kufanyiwa marekebisho licha ya kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha, hivyo tulijua hali halisi ya uwanja na mpinzani wetu," alisema Arafat.

Hatma ya Mechi ya Derby Tarehe 15 Juni

Arafat hakusita kuzungumzia pia kuhusu mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba SC iliyopangwa kuchezwa tarehe 15 Juni 2025, mechi ambayo awali ilipangwa kupigwa March 08.

Msimamo wa Yanga SC juu ya mechi hiyo, kwa mujibu wa Arafat, bado haujabadilika – hawatacheza.

"Waliopanga ratiba wanajua walichokimaanisha. Kama taasisi, Yanga SC ilishatoa msimamo wake juu ya hiyo mechi," alisema Arafat kwa msisitizo.

Akiendelea kufafanua, Arafat alieleza kuwa Yanga SC ina mialiko mingi ya kimataifa, na kuna uwezekano mkubwa kwamba timu hiyo haitakuwepo nchini katika tarehe hiyo.

"Yanga SC ina mialiko mingi kutoka Rwanda na Kenya, na pengine tarehe 15 tunaweza tukaenda Mombasa au Rwanda kuhudhuria mialiko hiyo," aliongeza.

Yanga imeweka ngumu kucheza mechi dhidi ya Simba Juni 15 wakiituhumu Bodi ya Ligi kuvunja kanuni kwa kuahirisha mchezo huo baada ya Simba kuingia mitini March 08

Yanga imeitaka Bodi iweke hadharani sababu za msingi zilizopelekea mchezo huo kuahirishwa na kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa mpira

Mabingwa hao wa Tanzania wameweka msimamo wa kutokuwa na imani na Bodi ya Ligi wakitaka wanaosimamia Bodi hiyo, Mwenyekiti Steven Mguto na Mtendaji Mkuu Almas Kasongo wajiuzulu

Lakini pia Wananchi wametaka wapewe alama tatu za mchezo huo ambao uliahirishwa baada ya Simba kuandika barua ya kugoma kucheza wakidai kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’