Zahera kuamua hatma ya Djako Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2018
Zahera kuamua hatma ya Djako Arafat
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano/Usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema tayari wamemaliza mazungumzo na mshambuliaji wa Wolaitta Dicha Djako Arafat na sasa jina lake wamelikabidhi kwa kocha Mwinyi Zahera ili kumuidhinisha iwapo asajiliwe au la.

Yanga ilianza mazungumzo na Djako baada ya mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho kati ya Dicha dhidi ya Yanga, mchezo ambao uliipa Yanga tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Djako raia wa Togo mwenye umri wa miaka 29 ndiye aliyefunga bao pekee la Dicha kwenye mchezo huo ambao Yanga ilifungwa bao 1-0.

Pia aliichachafya safu ya ulinzi ya Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam April 07 2018 ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.

Ndiye kinara wa kupachika mabao kwenye kikosi cha Dicha msimu huu, mpaka sasa akiwa na mabao saba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’