Hamdi kutumia kikosi kamili dhidi ya JKT Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2025
Hamdi kutumia kikosi kamili dhidi ya JKT Tanzania

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema hakuna nafasi ya kufanya makosa katika mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania hivyo wataingia katika mchezo huo wakiwa na kikosi kamili

Kesho Jumapili Yanga itashuka uwanja wa Mkwakwani, Tanga kumenyana na JKT Tanzania katika mchezo ambao Wananchi wanawania ushindi kutinga fainali ili kuwa na nafasi ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mfululizo

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Hamdi amesema atatumia wachezaji ambao wako fit kwa asilimia 100 ili kuhakikisha wanashinda

"Ni lazima tuingie katika mchezo huu tukiwa kamili kwa sababu hatutaki kukutana na matokeo ya kutuvunja moyo"

"Tunataka kushinda ili tuingie fainali hivyo nitakwenda kuweka kikosi imara. Nitatumia wachezaji ambao wako timamu kwa asilimia 100"

"Ninasema hivi kwa sababu hatuna chaguo jingine, hatutaki kukutana na 'surprise'," alisema Hamdi

Kikosi cha Yanga kilitua Tanga jana ambapo leo wachezaji watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Mkwakwani ambao utatumika hapo kesho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’