Ufafanuzi wa Ten kuhusu Salamba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2018
Ufafanuzi wa Ten kuhusu Salamba
Baada ya uongozi wa Yanga kutoa taarifa kuwa umeiandikia barua Lipuli FC juu ya kumtaka mshambuliaji wa timu hiyo Adam Salamba aongezwe katika kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, kumekuwa na upotoshaji juu ya swala hilo.

Jana Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten alitoa ufafanuzi ambapo amesema kimsingi si kwamba Yanga inataka kumsajili Salamba wakati huu.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya CAF hatua ya makundi, timu zilizotinga hatua hiyo zinaweza kuongeza wachezaji watatu (ambao hawajashiriki mashindano ya mwaka husika) kuongeza nguvu katika vikosi vyao ili mradi idadi ya wachezaji wote wasizidi 30.

Ten amesema wakati huu Yanga inamuhitaji Salamba na wachezaji wengine wawili ili kuongeza nguvu kikosi chake kinachoshiriki mashindano ya CAF na sio kumsajili kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa.

Ten amesema iwapo Yanga itataka kumsajili mchezaji huyo basi itafuata taratibu dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Litakuwa ni jambo la kushangaza kama uongozi wa Lipuli utamzuia mchezaji huyo kushiriki mashindano hayo ambayo huenda yakampa Salamba nafasi ya kuonekana Kimataifa.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Yanga kuongeza wachezaji kutoka timu nyingine kwenye kikosi chake kinachoshiriki michuano ya CAF hatua ya makundi.

Mwaka 1998 Yanga iliazima wachezaji watatu kutoka Simba ambao ni Monja Liseki, Shabani Ramadani na Alphonce Modest.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’