Nimeona huko mitandaoni baadhi ya mashabiki wa Simba wakimtupia lawana Mwenyekiti wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA) Injinia Hersi Said baada ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuupeleka Zanzibar mchezo wao wa fainali CAF CC dhidi ya RS Berkane utakaopigwa May 25
Inashangaza kidogo kwa sababu Hersi ambaye pia ni Rais wa Yanga, hahusiki kabisa na taratibu za mchezo huo
CAF wana taratibu zao ambazo wanazifuata pale wanapofanya maamuzi ya wapi mechi gani ichezwe na kwa nini
Kila mmoja anafahamu Serikali inafanya juhudi kubwa kuboresha uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuhahikisha unakuwa tayari kwa michuano ya CHAN inayoanza August mwaka huu
CAF walifanya ukaguzi na kujiridhisha na hali ya uwanja wa Mkapa na hatma yake kama utatumika katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha
Hersi anahusikaje hapo? Yeye ni Mjumbe tu wa Kamati ya utendaji ya CAF, maamuzi kuhusu ubora wa viwanja yanasimamiwa na Kamati maalum CAF
Lakini pia Uwanja wa New Amaan Complex ni moja ya viwanja bora hapa Tanzania na umekidhi vigezo vyote vya CAF
Kama nchi lazima tujivunie kuwa viwanja zaidi ya kimoja ambavyo vinakidhi vigezo vya CAF, ingekuwaje kama kiwnja kingekuwa kimoja, hiyo mechi si ingeenda kuchezwa nje ya nchi?