Yanga moja iko Moro nyingine Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2018
Yanga moja iko Moro nyingine Dar
Wakati nusu ya kikosi cha Yanga kikiwa mkoani Morogoro kikitokea Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar kesho, nusu nyingine iko Dar ikiendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sport.

Kocha Zahera Mwinyi ndiye anayekinoa kikosi kilichobaki Dar kikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Polisi wakati Shedrack Nsajigwa yuko na timu iliyoko mkoani Morogoro.

Uamuzi huo wa kugawa kikosi umepongezwa na wadau wa soka kwani unadhihirisha dhamira ya kocha Zahera anayetaka kuiona Yanga ikifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Kocha huyo amedhihirisha hahofii kufanya maamuzi magumu.

Uwamuzi wake unatoa nafasi kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kupata muda wa kutosha kujiandaa kabla ya kuikabili Rayon, Jumatano ijayo May 16.

Maamuzi yake yalikuwa ni ya lazima hasa ikizangiwa Yanga ilikuwa ikikabiliwa na michezo mitatu katika kipindi cha siku sita.

Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya Rayon ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
49m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’