Maxi, Pacome wapo sana Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2025
Maxi, Pacome wapo sana Jangwani

Kama kuna shabiki aliyekuwa akiamini Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli wanatimka Yanga kwa vile mikataba waliyonayo kwa sasa inamalizika mwisho wa msimu huu, basi pole yao kwani mabosi wa klabu hiyo wameamua kufanya kweli kuhakikisha nyota hao wa kikosi cha kwanza hawaendi kokote, huku wakishtua kwa kusaini mikataba mipya.

Pacome na Maxi waliosajiliwa msimu uliopita mikataba yao inaenda ukingoni na kulikuwa na tetesi kwamba mabosi wa Msimbazi walikuwa wakiwapigia hesabu ili kuhakikisha wanavuka mtaa kutua Simba, jambo lililowafanya vigogo wa Jangwani kukimbizana kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa.

Mabosi hao wa Yanga wameamua kumaliza mambo kiutu-uzima kwa kuwaita mezani wachezaji hao na kuwaongezea mkataba wa miaka miwili kila mmoja, ili kuendelea kukipiga katika kikosi hicho.

Maxi aliyesajiliwa kutoka AS Maniema ya DR Congo na Pacome aliyetokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast walisainishwa mikataba wa miaka miwili mara walipotua Jangwani ambayo inamalizika mwisho wa msimu huu.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha kuwa, tayari wachezaji hao wameshasaini mikataba mipya baada ya kufanya nao mazungumzo kwa muda mrefu wakishirikisha menejimenti inayowasimamia.

"Pacome bado ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa miaka mingine miwili zaidi, baada ya msimu huu kumalizika, isingekuwa rahisi kuachana na mchezaji mwenye kipaji kikubwa kama huyu," alisema bosi huyo wa juu wa Yanga na kuongeza;

"Kifupi haikuwa ishu ngumu kumbakisha, mchezaji mwenyewe alikuwa na amani ya kuendelea kuitumikia Yanga, ameshasaini mbele ya uongozi unaomsimamia sasa tunaangalia mbele zaidi. Ili uwe na timu lazima kuhakikisha unawabakiza wale wachezaji wako wazuri na wakubwa, Yanga haiwezi kuwapoteza wachezaji wake bora labda iamue kuwauza," alisema

Mapema msimu huu kulikuwa na presha kubwa kwa Pacome akitakiwa na klabu tatu za Kaizer Chiefs, Simba na Azam FC, ambazo kwa nyakati tofauti zilikuwa zinapiga hesabu za kumng'oa Yanga.

Ndipo Yanga ilipoamua kukaa mezani na mchezaji mwenyewe kwanza, baadaye ikamalizana na uongozi wake kwa makubaliano ya kumuongeza mkataba wa miaka miwili rasmi.

Hapo awali, gazeti la Mwanaspoti liliwahi kuandika kuwa, Simba ilikuwa na hesabu kali za kumsajili Maxi na bosi mmoja alipiga simu DR Congo akiulizia mkataba halisi wa mchezaji huyo

Wakati Simba ikisubiri majibu, uamuzi wa mwisho yulifanyika baada ya bosi mkubwa wa klabu ya AS Maniema, kumaliza kila kitu akiwaambia wasaidizi wake ndani ya klabu hiyo kuwa, hatma ya kiungo huyo kuondoka ndani ya Yanga labda itokane na timu hiyo kushindwana.

Maniema inayomilikiwa na Jenerali Amissi Kumba, aliyetoa msimamo huo akisema Yanga ni klabu rafiki na kufanya mazungumzo ya kumweka sokoni Maxi ni kama kuwakosea.

Hivyo, Yanga haikupata tabu kufanya mazungumzo ya kumuongeza mkataba Maxi, kwani tayari walishakuwa na uhakika naye tangu Januari

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’