Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam wakitokea Pemba ambako jana walifanikiwa kutwaa kombe la Muungano baada ya kuifunga JKU bao 1-0 katika mchezo wa fainali
Hilo ni taji la 7 kwa Yanga katika michuano hiyo iliyoanzishwa mwaka 1982, sasa ikiwa timu iliyoshinda taji hilo mara nyingi zaidi
Linakuwa taji la tatu Yanga kuchukua katika msimu huu ambao walianza na Toyota Cup kule Afrika Kusini na Ngao ya Jamii





ADVERTISE HERE