Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi wakati anatua kuchukua mikoba iliyoachwa na Sead Ramovic alisaini mkataba wa kuwatumikia Wananchi hadi mwishoni mwa msimu
Uongozi wa Yanga utaamua hatma yake mwishoni mwa msimu juu ya kumpa mkataba wa muda mrefu au
Hata hivyo mpaka sasa Hamdi ni kama amejitengenezea mazingira mazuri kwani kikosi chake kinafanya vyema
Katika mechi 15 alizoiongoza Yanga katika mashindano yote, ameshinda mechi 14 huku akitoka sare mchezo mmoja
Jukumu lililoko mbele yake ni kuhkikisha anaiongoza Yanga kutetea mataji mawili yaani ligi kuu ya kombe la Shirikisho la CRDB
Lakini pia kikosi cha Yanga kiko Pemba kikishiriki ligi ya Muungano, ni wazi kubeba ubingwa ni kipaumbele kwani itakuwa faida zaidi kwake
Hamdi alitua nchini kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuitumikia Singida Black Stars akidumu na timu hiyo kwa siku 36 tu kabla ya kutimkia Yanga
Uongozi wa Yanga ulilazimika kufanya uamuzi wa haraka kumuajiri baada ya kuondoka ghafla aliyekuwa kocha mkuu Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad