Mayele wa Pyramids Fc ndio yuleyule wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Apr 2025
Mayele wa Pyramids Fc ndio yuleyule wa Yanga

Straika wa mabao Fiston Mayele ameendelea kuthibitisha kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi katika bara hili kwa sasa akiwasha moto katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu ya Misri akiwa na Pyramids.

Mwamba huyu ni bidhaa iliyofanya vizuri katika Ligi Kuu Bara ndani ya misimu miwili akiwa na Yanga, na sasa inasumbua zaidi Misri, ligi namba moja kwa ubora barani Afrika.

Mabao mawili aliyofunga katika nusu fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini juzi yamemfanya Mayele afikishe mabao matano na kuwa kinara sawa na Emam Ashour wa Ahly na Ibrahim Adel wa Pyramids.

Mabao hayo yamechangia kuipeleka timu yake katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Pyramids itacheza na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.

Hii ni fainali ya pili kwa Mayele kwenye mashindano ya CAF baada ya ile ya msimu 2022/23 akiwa na Yanga alipoibuka mfungaji bora kwa mabao 7.

Kwenye msimu wake wa kwanza 2023/24 alicheza mechi 32 za mashindano yote na kufunga mabao 17 na asisti tano.

Licha ya ugeni wa ligi hiyo lakini namba zilionekana kumbeba Mayele kwenye msimu wake wa kwanza tu.

Akiendelea kupewa nafasi ndani ya kikosi hicho kilichosheheni nyota kibao msimu huu tayari amefunga mabao sita na asisti mbili kwenye mechi 19 za Ligi Kuu.

Mayele aliitumikia Yanga kwa misimu miwili akijiunga nayo msimu wa 2021/2022 akitokea AS Vita ya kwao DR Congo.

Nyota huyo alikuwa mhimili mkubwa wa Yanga na kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika michuano yote ile ya Ligi Kuu na mashindano ya CAF.

Katika msimu wa kwanza, staa huyo aliyesifika kwa staili yake ya kushangilia kwa ‘kutetema’, alishika namba mbili kwenye vinara wa upachikaji wa mabao wa Ligi Kuu akifunga mabao 16, nyuma ya kinara George Mpole aliyeifungia Geita Gold aliyemaliza mabao 17.

Hakuishia hapo, alifunga mabao mawili katika Kombe la Shirikisho (ASFC), na msimu huo huo alifunga bao moja kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Kiufupi katika msimu wa 2021/22, Mayele alifunga jumla ya mabao 19 katika Ligi Kuu, ASFC na Ngao ya Jamii.

Msimu uliofuata akafunga mabao 17 na kuibuka mfungaji bora sawa na Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ aliyekuwa Simba.

Akatwaa tuzo ya kibao ikiwamo Mchezaji Bora wa msimu sambamba na Bao Bora na pia alitajwa kwenye kikosi cha msimu cha Ligi Kuu 2022-23.

Msimu huo ndio aliisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga jumla ya mabao saba akifuatiwa na Rango Chivaviro wa Marumo Gallants aliyefunga sita.

Ikumbukwe pia kabla ya kudondokea katika Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilianzia kwenye Ligi ya Mabingwa na huko Mayele alifunga mabao saba akipiga hat-trick mbili dhidi ya Zalan FC ya Sudan na bao moja dhidi ya Al Hilal katika sare ya mabao 1-1, nyumbani kwa Mkapa kabla ya kutolewa kwa kuchapwa 1-0 ugenini pale Omdurman, Sudan.

Pia aliitungua Simba mabao mawili katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu huo, mechi iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 na pia kwenye ASFC ambako Yanga iliitwaa taji hilo akifunga mabao mawili.

Kiufupi msimu huo Mayele alifunga jumla ya mabao 35, kwenye Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika, ASFC na Ngao ya Jamii.

Kwa maana hiyo katika misimu miwili ambayo Mayele alicheza Yanga alifunga jumla ya mabao 54, rekodi ambayo inambeba hadi leo.

Baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa Yanga nyota huyo akatimkia Pyramids ambako sasa anajiandaa kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’