Unbeaten imefika 23

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
25 Apr 2025
Unbeaten imefika 23

Yanga inaendelea kuandika rekodi nyingine ya kibabe baada ya kucheza mechi 23 mfululizo bila kupoteza, zikiwamo 15 za Ligi Kuu Bara, nne ya Kombe la Shirikisho (FA) na nyingine nne za Ligi ya Mabingwa Afrika 

Rekodi zinaonyesha tangu Yanga ilipofungwa na MC Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza, haijapoteza mchezo wowote baada ya hapo

Kabla ya mechi hiyo, Yanga ilianza msimu kwa kucheza mechi nane mfululizo za Ligi Kuu na nne za raundi za awali za Ligi ya Mabingwa kwa kushinda zote na kutinga makundi ambapo ilianza kwa kufungwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Al Hilal na Mc Alger, huku katika Ligi ilitibuliwa na Azam iliyowafunga bao 1-0 kisha kulala 3-1 mbele ya Tabora United.

Ndipo baada hizo nne ilizopoteza mfululizo, Yanga ikajipanga na kucheza michezo 23 ya mashindano yote bila ya kupoteza na kati ya hiyo imeshinda 20 na kutoka sare tatu, ambapo safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho imefunga mabao 75 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 10.

Katika michezo hiyo 15 ni ya Ligi Kuu, ambapo imeshinda 14 na kutoka sare moja dhidi ya JKT Tanzania Februari 10, 2025, huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 52 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara sita.

Mingine minne ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, ikianza na sare ya bao 1-1 dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo kisha marudiano ikashinda 3-1, jijini Dar es Salaam, ikaifunga Al Hilal bao 1-0 na suluhu mbele ya MC Alger.

Katika michezo hiyo, safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao matano huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili pekee.

Michezo minne ni ya Kombe la Shirikisho (FA), ikianzia hatua ya 64 Bora kwa kuichapa Copco ya Mwanza mabao 5-0, kisha 32 Bora ikaichapa Coastal Union 3-1 na kutinga 16 Bora ilipoifunga Songea United 2-0 na kufuzu robo fainali.

Katika robo fainali, Yanga ikakutana na ‘Chama la Wana’ Stand United ikaichapa mabao 8-1 na kutinga nusu fainali itakayoicheza Mei 16 dhidi ya JKT TZ na kuifanya ifunge mabao 18 ya michuano hiyo, huku ikifungwa mawili na kufanya kiujumla imefunge 75 na kufungwa 10 kati ya michezo hiyo 23.

Ushindi wa mabao 4-0, ilioupata Yanga katika Ligi Kuu Aprili 21, 2025 dhidi ya Fountain Gate, ni wa nane mfululizo japo ni wa 15 kwa timu hiyo bila ya kupoteza tangu mara ya mwisho ilipochapwa 3-1, dhidi ya Tabora United, Novemba 7, 2024.

Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi aliyeanza kibarua kwa kulazimishwa suluhu na JKT na baada ya hapo kutopoteza mechi yoyote, amesema siri ya mafanikio hayo ni ubora wa kikosi

Msimu wa 2023/24, Yanga iliweka rekodi ya kucheza mechi 49 mfululizo bila ya kupoteza. Je Wananchi wataifikia tena rekodi hii?

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →