Mapema Jumatano, April 23 ilisambazwa barua feki katika mitandao ya kijamii iliyodai Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) wameupangia tarehe mchezo namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08
Hata hivyo TFF wamethibitisha barua hiyo ni feki kwani hawajaitoa wao. Ni wazi waliotengeneza na kusambaza barua hiyo walikuwa na ajenda yao
Lakini ukweli ni kwamba TFF, TPLB hawawezi kuupangia mchezo huo tarehe kabla ya maamuzi ya rufaa ya Yanga iliyofunguliwa CAS
Katika moja ya maombi yaliyowasilishwa na Wanasheria wa Yanga, ni kuzuia mchezo husika kupangiwa tarehe mpya kabla hukumu ya rufaa kutolewa
Maana yake ni kuwa haijalishi kesi hiyo itachukua muda gani, hatma ya mechi itategemea na hukumu itakayotolewa
Endapo Yanga itashinda madai yake ni wazi mechi hiyo haitachezwa kwa sababu TPLB watakuwa wamekosea katika uamuzi wao wa kuahirisha mchezo huo hivyo watapaswa kuipa Yanga alama tatu
Nafuu pekee ambayo inaweza kutoa mwanya kwa mechi hiyo kupangiwa tarehe ni endapo kama Yanga haitashinda madai yake