Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema ni lazima washinde mechi zote tatu zilizobaki ili kuweza kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Hamdi ambaye tangu alipotua Yanga hajapoteza mchezo wowote akishinda mechi 11 na kutoka sare mchezo mmoja, amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao katika kombe la Muungano lakini baada ya michuano hiyo watakuwa na kazi ya kufanya ili kuhitimisha msimu vyema
Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate, Yanga imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 70, alama 13 mbele ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 57
"Tunajua Simba wapo macho wanatazama mechi zetu wanasubiri tuteleze, wanasubiri makosa yetu na mara zote nawaambia wachezaji umuhimu wa alama tatu ni kitu ambacho hatupaswi kukisahau kila mchezo kwenye ligi hasa tunapoelekea ukingoni"
"Tunashukuru kwa mashabiki wanaokuja viwanjani nimefurahi kuona wakishangalia kwa hali na wachezaji wangu wamejitoa sana kuelekea hii michezo ya mwisho alama tatu ni muhimu sana"
"Kwa sasa hatupaswi kufanya makosa mchezo wowote ule kwasababu tunajua Simba yupo karibu na sisi," alisema Hamdi