Zikiwa zimesalia mechi tatu tu kwa Yanga kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya NBC 2024/25 mshambuliaji Clement Mzize anaongoza mbio za kuwania tuzo ya ufungaji bora
Mabao mawili aliyofunga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountan Gate jana, yamemfanya afikishe mabao 13 na kuwapiku Prince Dube na Jean Ahoua waliokuwa wakiongoza mbio hizo na mabao 12
Msimu huu Mzize amevunja rekodi yake ya mabao tangu apandishwe kikosi cha kwanza kutoka Yanga B misimu mitatu iliyopita, akifunga zaidi ya mabao 10
Jana alibeba tuzo ya nyota wa mchezo baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo ambao angeweza kufunga mabao zaidi ya matatu

ADVERTISE HERE