Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kila mwanachama na shabiki wa anapaswa wanahitaji kuwa wamoja na kuinga mkono timu yao ili kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizosalia ili kutetea ubingwa wao
Akizungumza katika uzinduzi wa Tawi la Yanga Manyara Raha mapema leo, Kamwe alisema kila mechi iliyobaki ni kama fainali kwani kila wanaposhuka dimbani hawachezi dhidi ya timu moja
"Kwa uzinduzi huu mkubwa naamini Tawi hili la Yanga Manyara Raha litakwenda kufanya vizuri na kuwa mfano wa Tawi bora hapa Babati na Manyara kwa ujumla. Ukiachia mbali uzinduzi wa Tawi hili lingine kubwa na la muhimu lililotuleta hapa ni mchezo wetu wa kesho dhidi ya Fountain Gate"
"Ndugu zangu tuko katika hatua za mwisho kabisa za kumaliza msimu huu wa 2024/25. Hawa tunaocheza nao kesho sisi tunawajua vizuri na aliyewatuma siku ya kesho tunamjua vizuri na nataka nizungumze vizuri mbele ya waandishi wa habari ili Ujumbe huu uwafikie na Wachezaji wetu"
"Hatua tuliyofika sasahivi kama Yanga kila mchezo kwetu ni vita kwasababu wote tunajua kila mechi yetu hatuchezi na mpinzani mmoja lazima tujiandae kweli kweli na naomba niwaombe wana Manyara na nyie mnalo jukumu la kupambana na sisi kushinda mchezo wa kesho"
"Hatujaja hapa na timu siku nyingi na ninaamini hamtakubali tuondoke hapa na matokeo mabaya"
"Sijaskia Wachambuzi na Waandishi wakiliongelea hili lakini Yanga mpaka sasa imeshakata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Klabu bingwa Afrika msimu ujao na ndio malengo na shauku ya kila mwanayanga ilipo, sisi Yanga hatuwezi kujiliza kwenye Kombe la Shirikisho ni Kombe ambalo kikanuni hakuna Bingwa wa nchi yoyote ile ameshiriki sisi huko tumeshavuka na malengo yetu yote yapo kwenye Klabu bingwa Afrika"
"Uongozi wa Klabu yetu chini ya Rais wetu Eng.Hersi Said wameshaanza kutengeneza timu kwa ajili ya msimu ujao maana malengo yetu yatakuwa ni makubwa zaidi. Twendeni tukashinde mchezo wetu wa kesho na watoto wanaotumwa tumwa kama hawa dawa yao ni kuwafunga kisawasawa," alitamba Kamwe