Kikosi cha Yanga kitaondoka jijini Dar es salaam Jumamosi, April 19 kuelekea mkoani Manyara tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate
Jumatatu, April 21 Yanga itashuka dimba la Tanzanite Kwaraa kumenyana na wenyeji wao Fountain Gate katika moja ya mechi za muhimu za kuhitimisha msimu huu
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itaondoka mapema asubuhi na treni ya SGR hadi mkoani Dodoma ambako wataunganisha kwa basi kuelekea Manyara
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga mkoani Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuwa tayari kwa mchezo huo ambao Yanga inahitaji kushinda
"Tunawaomba mashabiki wetu wa Manyara na mikoa ya jirani, tujitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuhakikisha timu yetu inapata ushindi"
"Timu yetu inatuhitaji sana mashabiki wakati huu ambao ligi inaelekea ukiongoni," alisema Kamwe
Yanga iko katika mkakati wa kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo, Wananchi wakisalia na mechi nne tu za kukamilisha malengo hayo
Mechi hizo ni dhidi ya Fountain Gate, Namungo Fc, Tanzania Prisons na Dodoma Jiji