Baada ya kukosa kushiriki ligi ya Muungano msimu uliopita, timu ya Yanga imetangaza kushiriki michuano hiyo ambayo itafanyika Visiwani Zanzibar
Kulingana na ratiba, April 23 michuano hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia robo fainali kwa mchezo kati ya JKU dhidi ya Singida Black Stars
April 24, Zimamoto itachuana na Coastal Union huku KMKM ikichuana na Azam Fc. Yanga itashuka dimbani Ijumaa, April 25 kumenyana na KVZ
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa Yanga itakwenda Zanzibar na kikosi chake kamili kwani wamepania kutwaa taji hilo la Muungano ambalo linashikiliwa na watani zao Simba wakilitwaa msimu uliopita
Klabu za Yanga, Azam Fc, Coastal Union na Singida Black Stars ndizo zinazoiwakilisha Tanzania Bara huku JKU, Zimamoto, KMKM na KVZ zikiiwakilisha Zanzibar
