Yanga iko mkoani Mbeya tangu jana na leo itashuka kwenye uwanja wa Sokoine kucheza na Prisons kwenye moja ya michezo yake ya kiporo ligi kuu ya Vodacom.
Yanga ilipowasili juzi kutoka nchini Algeria, kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera alipendekeza baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kutojumuishwa katika msafara unaokwenda mkoani Mbeya na Morogoro kwa ajili ya michezo dhidi ya Prisons na Mtibwa Sugar.
Sababu kubwa aliyotoa ni kwamba kutokana na ukaribu wa michezo hiyo ya ligi, inaweza kuathiri maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho ambapo Yanga itacheza na Rayon Sport May 16 2018.
Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Prisons, Yanga itacheza na Mtibwa Sugar May 13 mkoani Morogoro.
Baadhi ya wachezaji ambao wako mkoani Mbeya ni pamoja na Beno Kakolanya, Pato Ngonyani, Maka Edward, Baruani Akilimali, Yusufu Selemani, Godfrey Nyang'anya, Anthony Matheo na Amissi Tambwe
Wengine ni Thabani Kamusoko, Emmanuel Martin, Abdallah Shaibu "Ninja" na Yohana Nkomola

ADVERTISE HERE