Katika mchezo dhidi ya Azam Fc ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli ni miongoni mwa wachezaji 'waliokichafua' katika eneo la kiungo
Unaweza kusema yule Maxi wa msimu uliopita sasa amerejea baada ya kupita kipindi kigumu cha kusumbuliwa na majeraha msimu huu
Maxi amekuwa mchezaji wa timu zaidi msimu huu akihusika katika mabao 13, akifunga matano na kutoa pasi nane za mabao katika ligi
Kutokana na uhodari wake wa kukimbia eneo kubwa la uwanja, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi anamtumia kimkakati zaidi pasipo kumpa majukumu maalum
Umahiri wake katika kupiga mipira ya krosi umeinufaisha zaidi Yanga msimu huu kwani idadi kubwa ya mabao ya vichwa yaliyofungwa na Prince Dube, krosi zilitoka mguuni kwa Maxi
Yanga ikisaka taji la 31 na la nne mfululizo, Maxi ni miongoni mwa silaha muhimu katika kikosi cha Hamdi kukamilisha malengo hayo