Rais wa Yanga Injinia Hersi Said leo amepata nafasi ya kuonana na mmiliki wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir. Jim Ratcliffe na kumkabidhi jezi ya Yanga
Sir. Jim Ratcliffe yuko nchini kwa mwaliko rasmi wa serikali ambapo mapema alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es salaam
Sir Ratcliffe ni muumini mkubwa wa masuala ya uhifadhi akiwa anamiliki taasisi yake ya Six Rivers Africa inayosaidia miundombinu, tafiti na uendelezaji wa uhifadhi na utalii
Ujio wake kupitia mualiko wa serikali utaleta tija kubwa kwenye idara ya utalii nchini. Yanga imeahidi kushiriki kwa nafasi kubwa katika kutangaza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sera yake kubwa ya utalii



