Wakati msimu ukielekea ukiongoni Yanga tayari inapiga hesabu kali ya maboresho ya kikosi ili kuhakikisha inaendelea kufanya vyema katika mashindano ya ndani na Kimataifa
Kila mmoja anafahamu msimu huu hayakuwa malengo kuishia hatua ya makundi ligi ya mabingwa. Sasa mabosi wa Yanga hawataki kuona jambo hilo likitokea tena msimu ujao
Habari njema tayari Yanga imekata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao baada ya ushindi dhidi ya Azam Fc hapo jana
Kuna wachezaji wataondoka na wengine kusajiliwa kuchukua nafasi zao. Majina yameanza kutajwa, katika wale wanaoweza kutua miongoni mwao ni kiungo fundi Feisal Salum 'Fei Toto'
Taarifa za ndani zimedokeza kuwa Yanga imefikia katika hatua nzuri katika majadiliano ya kumrejesha mtoto nyumbani
Ukweli ni kuwa Fei aliondoka Yanga kutokana na mazingira ambayo yalitengenezwa nje ya uwanja mapema kabla ya Yanga kubaini
Yanga ilikuwa tayari kuboresha maslahi yake na sasa imerudi tena na kumuhakikishia mafanikio atayapata akiwa Jangwani
Lakini pia makubaliano ya kimkataba kati ya Yanga na Azam Fc wakati wa uhamisho wake yanaipa nafasi Yanga kumrejesha 'mwana' nyumbani
Aidha kuna juhudi kubwa zinafanyika kumpeleka Fei timu ile, lakini mkataba wake utawalazimu walipe fedha nyingi jambo ambalo ni gumu kutekelezwa
Wanasema hata vikombe huwa vinagongana kabatini ije kuwa binadamu? Yale yaliyojitokeza wakati wa sakata la uhamisho wake yanazungumzika na bila shaka mwafaka utapatikana...!
