Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amesema majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc jana hayakuwa makubwa hivyo matumaini yake ni kuwa atarejea uwanjani haraka
Pacome alifunga bao la kwanza katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa Azam Complex
Alishindwa kuendele na mchezo dakika ya 25 baada ya kuumizwa na beki wa Azam Fc Lusajo Mwaikenda
"Nilipata maumivu makali na kushindwa kuendelea na mchezo lakini nadhani sikuumia sana," alisema Pacome
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Pacome atafanyiwa vipimo kubaini aina ya majeraha na muda ambao anaweza kukaa nje ili kupona lakini ameonyesha kuwa na maendeleo mazuri baada ya mchezo hivyo matumaini ni makubwa atarejea uwanja mapema
Hii ni mara ya pili Pacome anapata majeraha katika mchezo dhidi ya Azam Fc. Msimu uliopita aliumia katika mchezo uliopigwa March 17 uwanja wa Benjamin Mkapa na kumfanya akose mechi muhimu za robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns akikaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu