Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amesema hali yake imeimarika na ameanza program maalumu ya mazoezi itakayomuwezesha kurejea dimbani karibuni.
Tambwe aliyeifungia Yanga bao moja pekee msimu huu kwenye michuano ya kombe la FA, ameeleza kukatishwa tamaa na majeraha ya goti yanayomsumbua ambayo madaktari wameshindwa kubaini tatizo.
Tambwe alianza kusumbuliwa na goti wakati Yanga ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii visiwani Zanzibar mwaka jana.
Mshambuliaji huyo anayeshikiria rekodi ya kufunga mabao 21 ya ligi kwa wachezaji wa nje, amesema goti hilo limekuwa likimsumbua kila anaporejea uwanjani lakini vipimo alivyofanyiwa na wataalamu mbalimbali vinaonyesha hana tatizo.
Hali hiyo ilimpelekea kwenda kwa viongozi wa kiroho kufanyiwa maombi maalumu.
Tambwe amesema anajisikia kuimarika zaidi baada ya maombi hayo na anaamini sasa atarejea akiwa kamili

ADVERTISE HERE