Tumejiandaa kuikabili Tabora United - Hamdi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2025
Tumejiandaa kuikabili Tabora United - Hamdi

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United ambao utapigwa kesho Jumatano, April 2 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Hamdi amesema amepata muda wa kuwasoma Tabora United, na ameaiandaa timu yake kuhakikisha hawarudii makosa yaliyopelekea wapoteze mchezo wa duru ya kwanza

Aidha Hamdi amewashukuru mashabiki wa Yanga wanaojitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao akiwaahidi siku ya kesho watafurahi

"Nianze kwa kuwashukuru mashabiki wote waliokuja kutupokea Uwanja wa ndege. Kwakweli kila siku wanazidi kunishangaza najiona kama Kocha mwenye bahati kuwa sehemu ya Klabu kubwa, Asanteni sana"

"Mchezo wa kesho kwetu ni mchezo muhimu sana na tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaondoka na alama hizi muhimu kwetu"

"Tumewafanyia kazi wapinzani wetu kwa umakini mkubwa kwasababu hatutaki kilichotokea nyuma kwenye mchezo wa kwanza dhidi yao kijirudie tena kesho, ni mchezo mgumu na kila timu inayokutana na sisi lazima wajaribu kucheza vizuri lakini sisi ni Klabu kubwa na haya ndiyo mazingira ya sisi kuhakikisha tunalidhihirisha hilo kwa kuondoka na ushindi," alisema Hamdi

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Kibwana Shomari amesema wanatambua umuhimu wa mchezo huo huku akiwataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuishangilia timu yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’