Kikosi cha Yanga Mapema Jumanne kinaondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Tabora tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya wenyeji wao Tabora United ambao utapigwa Jumatano katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Aidha katika sikukuu hii ya Eid El fitri, Yanga imeandaa chakula kwa ajili ya wakazi wa Tabora ambapo tukio hilo litafanyika uwanja wa Chipukizi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema takribani ng'ombe 20 wameandaliwa kwa ajili ya tukio hilo

ADVERTISE HERE