Aucho hatihati kuikosa Tabora United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Mar 2025
Aucho hatihati kuikosa Tabora United

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho amepata majeraha wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda

Aucho ambaye ni nahodha wa Uganda Cranes alikosa mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Guinea uliopigwa juzi jijini Kampala Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-0

Aucho alipata jeraha la misuli wakati wa maandalizi kuelekea mchezo huo na hivyo kumuweka kwenye hatihati ya kukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United utakaopigwa April 1 huko Tabora. 

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amekiri licha ya kuwa machaguo mengine katika eneo la kiungo, Aucho amekuwa na mchango mkubwa zaidi

Hamdi amesema anatamani kuona wachezaji wake wote wanarejea kutoka majukumu ya timu za Taifa wakiwa salama kwani anamuhitaji kila mchezaji katika nyakati hizi ambazo msimu unaelekea mwisho

"Bado tunapambana katika mbio za ubingwa wa ligi, hivyo mimi kama kocha natamani mastaa wangu wote wawe timamu ili niweze kuwa na kikosi kipana zaidi"

"Yanga ina wachezaji bora, ila kumkosa kiungo kama Aucho ni changamoto, kwani pengo lake sio rahisi kuzibika, licha ya wachezaji wenzake kuwa na bora pia," alisema

Viungo Duke Abuya na Salum Abubakar wametumika kwa nyakati tofauti pale Aucho anapokosekana

Msimu huu Aucho amekosa mechi tatu tu za ligi kuu ya NBC akicheza mechi 19 kati ya 22

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’