Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB), Simba na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa kuhudhuria
Wakati jitihada za kumaliza mgogoro huo 'mezani' zikiendelea, tayari Yanga imelipeleka suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) baada ya kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa na Bodi ya Ligi kuahirisha mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08
Bodi ya ligi iliahirisha mchezo huo baada ya Simba kutangaza haitacheza wakidai kuzuiwa kufanya maandalizi ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo huo
Kupitia matamko mbalimbali, Wanachama wa Yanga wameweka msimamo na wamewaagiza viongozi wao kutokuwa tayari kurejeshwa tena uwanjani kucheza mchezo huo wakitaka hatua zichukuliwe kwa mujibu wa kanuni