Ni wazi sasa yule aliyekosea na kupelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba kushindwa kufanyika March 08 amefahamika, kinachofanyika sasa na Bodi ya Ligi ni kuzuia adhabu kutolewa kwa kuzingatia kanuni
Kauli alizotoa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mnguto katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari akisisitiza busara na hekima kutumika kutatua mgogoro huo, inaonyesha wanakwepa kutumia kanuni kwa sababu wanafahamu kuna makosa yamefanyika na sasa wanamlinda huyo aliyefanya makosa asiadhibiwe
Mnguto anatoa mfano wa mgogoro wa mwaka 2021 akidai kuwa Yanga ingeshushwa daraja kama wangefuata kanuni, lakini anasahau kuwa Yanga iligomea mabadiliko ya muda wa mchezo kwa mujibu wa kanuni, kama Bodi ya Ligi wangeiadhibu Yanga ingekuwa uonevu kwa sababu Yanga ilisimamia kanuni
Kanuni zinaeleza wazi mabadiliko yoyote kuhusu muda wa mchezo yanapaswa kufanywa saa 24 kabla, Bodi ya ligi ilibadili muda wa mchezo saa 8 mchana saa 3 kabla ya muda uliopangwa awali
Wakati ule Yanga ilisimama kwenye kanuni na hata sasa Yanga imesimama kwenye kanuni. Kilichobadilika sasa ni kuwa Yanga imeweka msimamo kanuni ni lazima zifuatwe na sio busara kama ilivyofanyika nyakati zilizopita
Bodi ya ligi wameiambia Yanga hawawezi kuipa alama tatu, sasa ni vyema Wananchi wakaachwa waitafute haki yao katika mamlaka za juu
Kuwatisha kuwa wanapoteza mda na hawawezi kufanikiwa eti kwa kuwa walishindwa huko nyuma ni sawa na kupiga ramli tu
Kanuni za uendeshaji wa mpira wa miguu nchini ziko wazi, kilichofanywa na Simba na Bodi ya ligi ni kinyume cha kanuni
Kama wenye mamlaka wamegoma kutumia kanuni kuipa haki Yanga, CAS watazitumia kanuni kuipa Yanga haki yake