Mchezo maalum wa uzinduzi wa Airtel Stadium kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumatatu, March 24, utarushwa mbashara na Azam TV
Yanga imealikwa 'kunogesha' uzinduzi huo ambao mgeni rasmi ni Mhe Hamisi Mwinjuma (Mwana FA), Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao utahusisha wachezaji ambao hawako katika majukumu ya timu za Taifa
Nyota waliokwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa ni Djigui Diarra, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Duke Abuya, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Clement Mzize na Prince Dube
Mkufunzi wa Yanga Miloud Hamdi huenda akawaongeza baadhi ya wachezaji kutoka timu ya vijana Yanga U20