Klabu ya Yanga imewasilisha kesi Mahakama ya Kimataifa ya usuluhisi wa Michezo (CAS) ikipinga Bodi ya Ligi kuahirisha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba bila ya kufuata kanuni na kuitaka Mahakama hiyo iwapatie alama tatu kama kanuni zinavyoolekeza pale timu inapogoma kucheza mechi
Uamuzi wa Yanga kufungua kesi hiyo ni baada ya Bodi ya ligi kutupilia mbali maombi yao ya kupatiwa alama tatu baada ya Simba kuingia mitini March 08
Klabu ya Yanga imeeleza kutokuwa na imani na viongozi wa Bodi ya ligi na kuwa haitakuwa tayari kucheza mechi hiyo katika tarehe nyingine itakayopangwa
Kama Yanga itashinda kesi hiyo maana yake kanuni za uendeshaji wa ligi 2024/25 zitafuatwa, lakini pia adhabu kubwa inaweza kuwaangukia Simba kwa kukacha mchezo huo
Bodi ya ligi nayo inaweza kuwa matatani kwani ni dhahiri watakabiliwa na tuhuma ya kutumika kuhalalisha kile Simba walichokusudia kukifanya yaani kugomea mchezo huo
Ikumbukwe Simba ambayo ilishiriki taratibu zote za maandalizi kuelekea mchezo huo, ilitoa taarifa ya kutocheza usiku wa kuamkia Jumamosi ya March 08 wakidai klabu yao kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika ya uwanja wa Benjamin Mkapa
Asubuhi ya siku ya mchezo, Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Steven Mnguto alinukuliwa na vyombo vya habari akikisitiza mchezo huo upo na kuwataka mashabiki wa soka wandelee kukata tiketi
Taarifa ya Bodi ya ligi kuahirisha mchezo huo ilitoka majira ya saa 7 mchana wa siku ya mchezo yaani takribani saa 12 baada ya Simba kutangaza kugomea mchezo huo