Klabu ya Singida Black Stars, March 24 inatarajiwa kuzindua uwanja wao mpya ambao huenda wakaanza kuutumia katika mechi za kuhitimisha msimu huu
Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 5000-7000, utazinduliwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga
Wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, mechi hiyo pia itatumika kama sehemu ya maandalizi ya timu zote kuelekea mechi za kuhitimisha msimu
Yanga na Singida Black Stars tayari zimemalizana kwenye ligi, Yanga ikishinda mechi zote mbili
Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza na pia kushinda mabao 2-1 katika mechi ya pili

ADVERTISE HERE