Licha ya ushindani mkubwa uliopo katika ligi kuu ya NBC, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ana matumaini makubwa vijana wake wataendeza makali yao katika mechi zilizosalia ili kutetea ubingwa wao
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 58 baada ya mechi 22 huku Wananchi wakiwa na matumaini ya kuongeza alama nyingine tatu kufuatia watani zao Simba kuingia mitini katika mchezo uliopaswa kupigwa March 08
Kuna mechi 7 zimesalia kwa Yanga kuhitimisha msimu ambapo mechi tatu zitapigwa nje ya jiji la Dar es salaam na nyingine nne kupigwa Dar
Mechi zilizobaki ni dhidi ya Tabora United (A), Coastal Union (H), Azam Fc (A), Fountan Gate (A), Namungo (H), Prisons (A) na Dodoma Jiji (H)
Miloud amesema kila mchezo una ushindani mkubwa jambo ambalo litawafanya wapambene ili kupata matokeo mazuri
"Ushindani ni mkubwa na wachezaji wanajituma kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo nina amini kwamba tutaendelea kuwa kwenye ushindani katika mechi zinazofuata," alisema Hamdi
Nyota wa Yanga walipewa mapumziko ya siku 6 na wanatarajiwa kurejea mazoezini mwanzoni mwa wiki ijayo kujiandaa na mechi hizo za lala salama