Unaweza kusema kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli sasa yuko katika nyakati bora msimu huu akiendelea kufunga na kutoa pasi za mabao
Jana Maxi aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa kombe la Shirikisho la CRDB na kutinga hatua ya 16 bora
Katika mchezo huo Maxi alifunga mabao mawili huku bao la tatu likifungwa na Clement Mzize
Pengine Maxi angeweza kuondoka na mpira 'hat-trik' kama sio moja ya majaribio yake kugonga mwamba katika kipindi cha kwanza
Maxi alianza vyema msimu lakini baadae akapata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa zaidi ya wiki sita
Tangu arejee kutoka katika majeraha, kwenye ligi kuu Maxi amefunga mabao mawili na kutoa assist 4 na hivyo kuwa na jumla ya mabao matano na assist 6 msimu huu
Mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu lakini tayari makubaliano ya mkataba mpya yamefikiwa