Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesemaa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki yuko kamili kuwatumikia Wananchi katika mchezo wa kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa leo katika uwanja wa KMC Complex
Aziz Ki alikuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga ambapo alikosa sehemu kubwa ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao hata hivyo haukufanyika
"Ukimuondoa Yao Kouassi, wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo dhidi ya Coastal Union"
"Tunafahamu tunakwenda kukutana na timu ngumu, Coastal Union ni miongoni mwa timu bora katika ligi yetu"
"Tutachukua tahadhari zote kuelekea mchezo huu kwani tumeona baadhi ya timu kubwa zimeondoshwa katika hatua hii na zinazoonekana kuwa timu ndogo," alisema Kamwe
Mshindi wa mchezo wa leo atatinga hatua ya 16 bora ambapo katika hatua hiyo atachuana na Songea United inayoshiriki ligi ya Championship