Tuko juu kwa tofauti ya alama 7 - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2025
Tuko juu kwa tofauti ya alama 7 - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba baada ya kile kilichotokea jana, Yanga imeongeza alama tatu na sasa iko juu ya msimamo kwa tofauti ya alama 7

Kabla ya sintofahamu ya mchezo dhidi ya Simba, Wananchi walikuwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 58 huku watani zao Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 54

"Alhamdulillah .. Derby Imekwisha na Yanga Tunaongoza Ligi Kuu kwa Tofauti ya pointi 7," aliandika Kamwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Yanga ilifika dimba la Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo huo lakini Simba hawakutokea

Kikosi kiliiingia dimbani majira ya saa 11 Alasiri na timu kukamilisha taratibu zote za mchezo huo na baadae kuondoka uwanjani baada ya kukamilika kwa muda wa kusubiri wa mujibu wa kanuni

Yanga inaamini inastahili kupewa alama tatu na mabao matatu na sio mchezo huo kupangiwa tarehe nyingine kwa sababu hakukuwa na sababu zozote za msingi kupelekea bodi ya ligi kutangaza kuahirisha

Yanga imeapa kama haitapata haki yake katika mamlaka za ndani basi watakwenda kuidai kwenye mamlaka ya juu ambayo ni FIFA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’