Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani ametaja sababu ya kuzima simu yake siku chache zilizopita ilikuwa kukwepa usumbufu kutoka vilabu vya Simba na Azam FC vinavyotaka kumsajili.
Yondani amesema amekuwa akisumbuliwa na timu hizo zinazomuwania amwage wino kuzitumikia msimu ujao.
Katika mazungumzo yake na viongozi wa Yanga waliofika nyumbani kwake kumjulia hali juzi, Yondani ameweka wazi kuwa anataka amalizie soka lake akiwa katika klabu ya Yanga.
Mkataba wa beki huyo wa kuitumikia Yanga unamalizika mwezi huu na tayari uongozi wa Yanga umeanza juhudi za kumpa mkataba mpya.

ADVERTISE HERE