Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Job alisema wanafahamu umuhimu wa mchezo huo hivyo wamejiandaa na watapambana ili kuhakikisha wanashinda
"Kwa niaba ya wachezaji wenzangu niseme tu sisi tuko tayari kwa mchezo huu. Tunatambua umuhimu wa mchezo hivyo tutapambana ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri "
"Tunajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu hata wapinzani wetu wanafanya vizuri, safu yao ya ushambuliaji ni nzuri hivyo jukumu letu ni kuhakikisha tunalinda vizuri kuepukq kuruhusu bao"
"Hii ni mechi ya Derby ambayo inahitaji matokeo, sisi tunahitaji pointi tatu na wapinzani wetu nao wanahitaji pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa. Hivyo tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini sisi tumejiandaa vyema na tutaipambania nembo ya Yanga ili kushinda," alisema Job