Mapema leo Rais Yanga Injinia Hersi Said alikabidhi mfano wa hundi ya Tsh 100,000,000 Kutoka kwa Yanga na GSM Foundation kwenda Hospitali ya Amana
Ni katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuokoa uhai wa mama na mtoto
Hersi amemshukuru Waziri wa Afya Mh. Jenista Mhagama kwa kushiriki tukio hilo huku akitoa ahadi ya kuendelea kuunga mkono jithada za Serikali
"Ahsante Mh. Waziri wa AFYA JENISTA MHAGAMA kwa uwepo wako kushuhudia makabidhiano hayo"
"Klab yetu kwa kushirikiana na wadhamini wetu GSM FOUNDATION tutaendelea kuunga mkono jitahada za serikali yetu chini ya Mh. Rais, Daktari Samia Suluhu Hassan kuleta maendeleo kwa wananchi katika sekta hii muhimu ya AFYA, hususan eneo la MAMA NA MTOTO," alisema Hersi


ADVERTISE HERE