Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Karim Boimanda amesema mwamuzi wa mechi ya ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba itakayopigwa Machi 8, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ni Ahmed Arajiga
Arajiga atasaidiwa na waamuzi wasaidizi Kassim Mpanga na Mohammed Mkono huku mwamuzi wa akiba akiwa Amina Kyando

Arajiga kwa sasa amejipambanua kuwa mwamuzi bora nchini hivyo hatua ya kupewa kuchezesha mechi hiyo imepongezwa na wengi
Hiyo itakuwa mechi ya 7 Arajiga anaichezesha Yanga msimu huu ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya Kariakoo Dabi pia kwa msimu huu
Ni Arajiga aliyechezesha mechi zote mbili za ligi msimu uliopita Yanga ikishinda zote

ADVERTISE HERE