Tatizo ni timu, sio mchezaji mmoja mmoja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2018
Tatizo ni timu, sio mchezaji mmoja mmoja
Mchezo wa jana dhidi ya USM Alger umedhihirisha madhaifu ya kikosi cha Yanga hasa katika umiliki wa mpira kwenye michezo yenye presha kubwa.

Kwa muda mwingi USM Alger ilikuwa imeweka kambi kwenye lango la Yanga kwa kuwa ilikuwa vigumu kwa wachezaji wa Yanga kutunza mpira hata kwa sekunde 15.

Yanga ilipiga mashuti mawili pekee kwenye lango la USM wakati waarabu hao walipiga mashuti 19 langoni kwa Yanga.

Iko hivi, kadiri unavyomkaribisha mpinzani kwenye lango lako unaongeza uwezekano wa wewe kufanya makosa na kufungwa.

Kumlaumu mlinda lango Youthe Rostand kuwa alifanya makosa ya kizembe haiwezi kuwa sawa kwani presha ya mchezo ilikuwa ni kubwa.

Rostand amekuwa akiibeba Yanga kwenye michezo mingi tu, kufungwa kwake mabao manne hakutokani na udhaifu wake, bali ni udhaifu wa timu kwa ujumla.

Ndio, anayo makosa yake kama mlinda lango lakini yeye hawezi kuwa sababu pekee ya Yanga kufungwa jana.

Kama Yanga ingepunguza mashambulizi langoni mwake ni dhahiri ingepunguza uwezekano wa kufanya makosa.

Njia sahihi ya kujilinda ni kumuweka mbali ya lango mpinzani wako kwa kumshambulia yeye na sio kumpa nafasi ya kukushambulia kwa muda mrefu kama ilivyokuwa jana.

Kwa ujumla Yanga ilishindwa kwenda na kasi ya USM Alger.

Waarabu hao wangeweza kufunga zaidi ya mabao manne kama washambuliaji wake wangekuwa makini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
47m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’