Yao anaendelea kuimarika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2025
Yao anaendelea kuimarika

Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti wiki chache zilizopita

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Yao ameanza kutembea 'kawaida' ikiwa hatua nzuri kuelekea kurejea kwake uwanjani

Hata hivyo Kamwe amesema Yao hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Simba siku ya Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

"Yao anaendelea kuimarika sasa akitembea kawaida pasipo usaidizi wa magongo. Najua mashabiki wa Yanga wana shauku kubwa kutaka kujua kama Yao ataweza kucheza siku ya Jumamosi"

"Niwaambie tu, yuko katika hatua nzuri katika 'recovery' lakini bado hayuko tayari kucheza mpira hivyo tufahamu Jumamosi hatakuwa sehemu ya kikosi," alisema Kamwe

Yao tayari amekuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne baada ya upasuaji ambapo anatarajiwa kuwa nje kwa wiki sita kabla ya kuanza mazoezi ya kumrejesha tena uwanjani

Israel Mwenda na Kibwana Shomari wamefanya kazi nzuri katika kipindi chote ambacho Yao amekosekana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’