Juzi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi alimuweka nje kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua
Pacome ana kadi mbili za njano, kama angetumika katika mchezo huo na kupata kadi nyingine, angekosa mchezo utakaofuata dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Sasa habari ziwafikie! Pacome atakuwepo Jumamosi kuendeleza ubora wake msimu huu
Mpaka sasa Pacome amefunga mabao 7 na kutoa assist 7 akiwa miongoni mwa wachezaji waliohusika katika mabao mengi kwenye kikosi cha Yanga
Ukizungumzia timu yenye safu bora ya ushambuliaji basi utaitaja Yanga iliyofunga mabao 58 katika mechi 22
Eneo la mbele limetoa uwiano mzuri wa kufunga na kutoa pasi za mabao. Pacome mabao (7), Mzize (10), Dube (10), Aziz Ki (7) na Maxi (5)