Tumewazidi kila kitu! Ndio kauli na tambo za mashabiki wa Yanga zinazosikika kwa sasa baada ya hapo jana kuishuhudia timu yao ikiendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji
Kwa sasa Yanga iko pale juu ya msimamo ikitamba na alama 58 alama 7 mbele ya watani zao Simba wenye alama 51
Ile kauli ya kila mmoja ashinde mechi zake imedhihiri sasa kwani mfululizo wa kushinda mechi umeifanya Yanga irejee katika nafasi yake huku Wananchi wakiapa hawashuki tena chini 'ngo hadi msimu utamatike
Mabao 58 na pointi 58 kileleni huku Wananchi wakiwa wameruhusu mabao 9 na hivyo kuwa na uwiano wa mabao 49 (GD)
Yaani Simba watahitaji kufunga mabao 14 katika mechi zao mbili ili kufikia idadi ya mabao ya Yanga
Kazi iliyobaki kwa Yanga ni kuhakikisha Jumamosi inashinda mchezo dhidi ya Simba ili kumaliza kabisa kelele za ipi ni timu bora nchini
Licha ya Yanga kushinda mara nne mfululizo dhidi ya watani zao, bado kuna wabishi wachache hawataki kukubali ubora wa Yanga