Baada ya kuoa wapo waliodhani kasi ya Stphane Aziz Ki itapungua lakini ndio kama kazaliwa upya!
Akiingia katika kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji leo, Aziz Ki ndiye aliyeimaliza mechi hiyo akifunga mabao mawili muhimu yaliyoihakikishia Yanga ushindi wa mabao 3-0
Ki sasa amefikisha mabao 7 nyuma ya Prince Dube na Clement Mzize kwa tofauti ya mabao matatu tu
Taratibu Aziz Ki anaingia katika mbio za kuwania ufungaji bora huku pia akiendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga na kutengeneza mabao
Aziz Ki pia ametoa pasi 7 za mabao na hivyo kuhusika katika mabao 14 msimu huu
Ni Dube aliyehusika katika mabao mengi zaidi katika kikosi cha Yanga na katika ligi msimu huu akihusika katika mabao 17

ADVERTISE HERE