Kabla ya mchezo dhidi ya Mashujaa Fc, zilianzishwa propaganda kuwa kiungo Clatous Chama hana furaha kutokana na nafasi yake duni katika kikosi cha Yanga
Baadhi wachambuzi wakaenda mbali zaidi na kudai mwamba huyo wa Lusaka alifanya makosa kuikacha Simba na kujiunga na Yanga ambayo imemfanya ashuke kiwango
Hata hivyo dakika zake 25 katika mchezo dhidi ya Mashujaa Fc zimetosha kumaliza mijadala hiyo kwani alizitumia vyema kufunga mabao mawili na kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0
Mabao hayo yamefanya aongeze idadi yake ya mabao msimu huu sasa akifikisha mabao matatu na assist 2
Msimu huu nyota wa Yanga wanawaumbua baadhi ya 'wachambuzi wa mchongo' kila wanapoanzisha propaganda dhidi yao
Clement Mzize, Stephane Aziz Ki, Prince Dube, Pacome ni miongoni mwa waliokabiliana na ukosoaji mkubwa nje ya uwanja lakini sasa wako katika orodha ya wanaofanya vyema msimu huu
Mzize na Dube ndio vinara wa mabao huku Dube akiwa mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi msimu huu