Hafla ya ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobeto ilifanyika jijini Dar es salaam jana na kuhudhuriwa watu mashuhuri
Wachezaji wa Yanga walimuunga mkono mwenzao na kunogesha hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa The Superdome Masaki.
Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Yanga wakati wa kutoa zawadi, Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine alitangaza kuituza familia ya Aziz Ki na mkewe Tsh Milioni 50
Nae Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe akaweka msisitizo kuwa kiasi hicho cha fedha tayari kimeingizwa katika akaunti ya Aziz Ki hivyo Hamisa anapaswa kujua namba ya siri ya akaunti ya mumewe!
"Nataka kuliweka hili sawa. Hii sio ahadi kiasi cha Sh 50 milioni kimeshaingizwa kwenye akaunti ya Aziz Ki, na Hamisa kitu cha kuzingatia ni kujua paswedi maana pesa tumeshaitoa," alisema Kamwe
Tukio hilo limehitimisha shamrashamra za harusi ambayo kwa takribani wiki nzima ilikuwa ni habari kubwa