Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi imewapeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe na Ofisa Habari wa Kagera Sugar Hamis Mazanzala kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili kupitia machapisho yao katika kurasa za mtandao wa Instagram
Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa viongozi na maofisa wa klabu kuwa wanazuiliwa kwa mujibu wa kanuni kutoa maandiko au matamshi chonganishi ama yanayoweza kuchafua taswira ya ligi na mpira wa miguu kwa ujumla
ADVERTISE HERE