Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametamba kuwa wataendelea 'kuhusika' katika mechi za Yanga hadi mwisho wa msimu
Ahmed alitoa kauli hiyo baada ya Simba kupata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi wakifaidika na suluhu ya bila kufungana ambayo Yanga waliipata dhidi ya JKT Tanzania
Kauli hiyo inadhihirisha ni kwa kiasi gani mechi zilizobaki kwa Yanga zitakuwa ngumu kwani kila mpinzani ambaye atacheza na Yanga, akishinda au kutoka sare 'ana-hamasa' kutoka upande wa pili
Wapinzani wamewekeza katika kushinda mechi zao na pia kuhakikisha Yanga haishindi mechi zake
Pengine sasa ni wakati kwa viongozi wa Yanga nao kuwa macho, mechi zilizobaki kuhitimisha msimu huu ni kama vita!
Ukiona mpinzani wako anatamba hadharani anahusika katika mechi zako, unapaswa kuongeza umakini na kuhakikisha unaziandaa silaha zako vyema
Kwani katika mechi hutakuwa ukicheza na timu moja, kuna wapinzani wengine hawaonekani lakini nao watakuwa kazini..!