Februari 14 katika uwanja wa KMC Complex Yanga inakabiliwa na mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya KMC
Ukiangalia ratiba ya Yanga ya mechi nne zilizobaki kuhitimisha mwezi Februari, utabaini vijana wa kocha Miloud Hamdi wanapaswa kufunga mkanda kwelikweli ili kuhakikisha alama zotee 12 zinapatikana kabla ya kuwavaa watani zao March 08
Droo dhidi ya JKT Tanzania jana inapaswa kuwakumbusha wachezaji wa Yanga kuwa kila mechi iliyobaki ni kama fainali, hakuna tena mechi nyepesi
Yanga itarajie kukutana na upinzani ambao pengine haukuonekana katika mechi zilizopita
Unaweza kusema mechi tano zijazo zinaweza kutoa taswira ya hatma ya ubingwa msimu huu
Baada ya kuikabili KMC Feruari 14, Yanga itapumzika kwa siku tatu tu na kurejea tena KMC Complex Februar 17 kuikabili Singida Black Stars
Februari 23 Yanga itakuwa Kigoma kuikabili Mashujaa Fc kisha kuelekea Mwanza kuikabili Pamba Jiji, February 28
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba ukitarajiwa kupigwa March 08